Bunge la Marekani limewachagua viongozi wake wapya, wiki mbili na nusu tu kabla ya rais mteule Joe Biden kuchukua madaraka rasmi. 

Kwa mara nyingine Baraza la Wawakilishi limemchagua Nancy Pelosi kuwa Spika wake, japo kwa kura chache ikilinganishwa na muhula uliopita. 

Kwa uchaguzi huo Bi Pelosi mwenye umri wa miaka 80 anaendelea kushikilia mojawapo ya ofisi zenye mamlaka makubwa kabisa nchini Marekani.

 Hata wajumbe wa Baraza la Seneti walikula kiapo, lakini uongozi wa baraza hilo utajulikana bayana baada ya uchaguzi wa marudio wa majimbo mawili ya ubunge katika jimbo la Georgia ambao unafanyika kesho Jumanne. 

Matokeo ya uchaguzi huo ndio yataamua uwezo atakaokuwa nao rais mpya katika kupitisha sera zake.