DESEMBA 4, 2020, Gazeti namba moja la burudani na habari za mastaa, IJUMAA ndilo liliripoti kwa mara ya kwanza kuhusu tetesi za kwamba Mzee Abdul si baba mzazi wa mwanamuziki Diamond Platinumz. Baaada tu ya kuzinyaka nyepesi hizo zikiwa za moto, GAZETI IJUMAA lilimtafuta na kumfanyia mahojiano EXCLUSIVE Mzee Abdul kuhusu tetesi hizo ambapo alicharuka vibaya san ana kuzungumza maneno makali.


 
Lakini leo, January, 15, 2021, Mama Diamond na Ricardo Momo wamethibitisha hilo kupitia WASAFI FM kwa kusema Mzee Abdul si baba yake na Diamond, kwani Baba mzazi wa Diamond ni baba yake na Ricardo Momo, na wakati Mama Dangote alipoanza mahusiano na Mzee Abdul tayari alikuwa na ujauzito wa baba yake na Ricardo Momo.