Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez juzi usiku alifanyiwa fujo katika Uwanja wa Amani mjini hapa, muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza kufanya mazoezi uwanjani hapo.
tiketi barbara
Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez juzi usiku alifanyiwa fujo katika Uwanja wa Amani mjini hapa, muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Akizungumza na Mwanaspoti jana, Barbara alisema alifanyiwa fujo wakati akiswali swala ya Ishah saa mbili usiku katika uwanja huo, baada ya timu kuondoka.


“Wakati naswali walikuja watu wakaanza kunivuta, kunipiga na kuvuta mtandio wangu. Waliniumiza sana,” alisema mtendaji huyo aliyehusisha tukio hilo na mchezo wa fainali kati ya Simba na Yanga uliochezwa jana usiku.

Alisema baada ya tukio hilo aliripoti katika Kituo cha Polisi Ng’ambo alikofunguliwa jalada lenye namba NGB/RB 247/2021, ambapo watuhumiwa kadhaa walikamatwa na kuwekwa ndani usiku huohuo. Gazeti hili lilifika katika kituo hicho ambapo polisi walikiri kupokea malalamiko na kufungulia jalada la shambulio la mwili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadhi Juma Haji alisema hana taarifa juu ya tukio hilo.