Ikumbukwe kuwa Harmonize akiwa nje ya nchi ambapo alikuwa nchini Ghana siku ya Januari 2, 2021, alitangaza kutafuta mwimbaji wa kike ili amshirikishe kwenye ngoma yake na baada ya mapendekezo ya watu alitangaza kumtafuta mwimbaji wa nyimbo za kurudia ‘Cover’, aitwaye Abella na alifanikiwa kumpata.Baada ya kukutana naye jana ofisi za Konde Gang Anjella alikuja na mzazi wake na hapo ndipo walipoonana uso kwa uso na Harmonize.

Kila mmoja alipata nafsi ya kuongea na baada ya hapo Harmonize alimuomba Anjella aimbe angalau nyimbo mbili cover anazoimba na alifanikiwa kuimba ngoma ya Ruby lakini harmonize alimuomba aimbe nyimbo yoyote ya Nandy na alifanya hivyo.