Misri imeanza kutoa chanjo ya COVID-19 jana, hivyo kuwa moja kati ya Nchi za Afrika ambazo zimeanza kuwachanja Raia wake dhidi ya virusi vya corona.
Daktari mmoja pamoja na muuguzi mmoja ni miongoni mwa Watu wa kwanza kupewa chanjo ambayo imetengenezwa na kampuni ya China Sinoopham.
Taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya Watu ambayo ni zaidi ya milioni 100, lilipokea shehena ya kwanza chanjo mwezi Disemba, Waziri wa Afya Hala Zayed amesema leo kwamba chanjo hiyo itatolewa kwa Wahudumu wote wa afya bila malipo.
Misri imerekodi maambukizi 160,000 ya Corona pamoja na takriban vifo 9,000 tangu janga la Corona lianze.