Kuna mengi yanaendelea kuibuka toka kwenye faili la talaka ambalo Nicole Young alilifungua mahakamani kudai talaka kwa Dr. Dre.


Ukiacha tuhuma za kudai kuwahi kupigwa ngumi mara mbili kichwani na kisha kufungiwa chumbani Mwaka 2016, Nicole amefunguka pia kuwahi kushikiwa bastola kichwani mara mbili, mwaka 2000 na 2001.


Dre amekanusha tuhuma hizo kwa kusema "Katika muda usiofahamika, sijawahi kumpiga wala kumtishia Nicole kuhatarisha usalama wake." Maelezo ambayo Nicole ameyakana na kusema vipigo vile vilipelekea apate msongo wa mawazo na anaamini Mahakama itatumia hiyo kama sababu ya kumpatia ushindi kwenye shauri hilo ambalo anadai pesa za matunzo na matumizi.


Wakati hayo yote yakiendelea, Dre bado yupo hospitali mara baada ya kupata tatizo kwenye ubongo na kukimbizwa hospitali mnamo Januari 4 mwaka huu. Wakati pia yupo hospitali, mwanasheria wa Dre alikubali ombi la kumlipa Nicole ($2 million) kama pesa za matunzo kwa miezi michache ijayo.