Makamu Wa Rais Mhe. Samia Awafariji Majeruhi Wa Ajali Ya Treni Dodoma
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewatembelea majeruhi wa ajali ya treni katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ambapo ametoa maagizo kwa mkoa kuhakikisha wanasaidiwa kufika makwao mara watakapopata nafuu.
Samia alitoa kauli hiyo baada ya kuzunguka katika wodi zote walikolazwa majeruhi hao na kuzungumza nao lakini akasema ameridhishwa na hali zao pamoja na huduma wanayopata wagonjwa hao.
Kiongozi huyo amefika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma mapema saa moja asubuhi na mbali na kuzungumza na majeruhi wa treni lakini amezungumza na wagonjwa wengine akiwafariji.