MKALIwa Ngoma ya Nakupenda, Alikiba amesema kuwa ishu ya kutoa albam kwa mwaka huu ipo kwa asilimia zaidi ya 100 na watu watarajie kuipata kabla haijafika mwezi wa sita.

 

Kiba alisema imepita miaka zaidi ya 10 tangu alipotoa albam ya Alikiba For Real, hivyo anaona ni wakati sahihi sasa wa kukata kiu ya mashabiki wake waliosubiri kwa muda mrefu sasa.

 

Huku akiongeza kuwa maandalizi kuelekea kwenye jambo hilo yapo vizuri zaidi.Kiba aliliambia Championi Jumamosi kuwa: 

 

“Watu wamesubiri albam yangu kwa zaidi ya miaka 10, nafikiri sasa ni wakati sahihi wa kufanya jambo kwa watu wangu wa nguvu. Haitafika hata mwezi wa sita mzigo utakuwa sokoni.”

 

Kiba ambaye anamiliki albam mbili, Cinderella ya mwaka 2007 na Alikiba For Real iliyotoka 2009, kwa sasa anatamba na mkwaju wa Nakupenda akiwa na Dj Sbu.