Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza kusitisha kwa muda mafunzo ya jeshi hilo ya kujitolea kwa mwaka 2020/2021 mpaka hapo itakapotangaza tena.
Kutokana na kusitishwa kwa Mafunzo hayo JKT imewataka vijana walioripoti makambini kurejea majumbani na wale ambao hawajaripoti wasiende kuripoti.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena, wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi za makao makuu ya jeshi hilo.