WATU wengi nchini wamekosa ajira  kwa sababu ya makosa wanayoyafanya wakati wa kuandika CV zao.

Kumbuka,  makampuni  karibia yote yanayotangaza nafasi za kazi hupokea wastani wa maombi 200-500 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. 

Hivyo, CV yako lazima ikae vizuri ili kumshawishi mwajiri. Utaratibu wa kuomba kazi unaweza ukawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji uwatumie CV.

CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa kiundani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.

Mambo yafuatayo yatasaidia kuifanya CV yako iwe bora na hivyo, kukusaidia kupata interview za kazi.

👉Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.

Kwa mfano, kama kazi inaweka umuhimu kwenye ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa matangazo, hakikisha CV yako ina kazi zote zilizohitaji matumizi ya mitandao ya kijamii.

👉Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uyatumie kwenye CV
Usichukue sentensi nzima kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.

👉Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika nayo. 

Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.

👉Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia kufanya kazi unayoomba.

==>Format/Staili inayotumika zaidi kwenye kuandika CV:
   1. Lengo la CV na ujuzi wako
    2.Ujuzi wako wa kazi
   3. Mafanikio maalum
   4. Elimu
   5. Ujuzi muhimu binafsi

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Angalizo:
  1.  Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
  2.  Tumia size 9 – 12 ya herufi
  3.   Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
  4.   CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
  5.   Usitumie sentensi ndefu
  6.  Hakikisha CV yako inasomeka kiurahisi na inawasilisha   mafanikio yako kwa uwazi.
  7.  Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu rudi nyuma.
   ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 
   ==>.Hakikisha Yafuatayo:
1.Ukiwa unaandika jina la kampuni uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. 
2.Eleza kwa ufupi kampuni yao inahusika na nini. 
3.Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na mwaka).  
4.Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu yako kwenye hiyo kampuni.
5.Usidanganye

👉Maandalizi ya Mwisho

1.Pitia kila kitu kwa mara ya mwisho
 -Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosa yako.

2.Mpe Rafiki  yako apitie CV
-Muombe rafiki yako apitie CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba maelezo yaliyoelezwa humu yatakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.