IGP Sirro : Makosa Ya Usalama Barabarani Yamepungua Kwa Asilimia 34
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema makosa ya ajali barabarani nchini yamepungua kwa asilimia 34 kutokana na madereva wengi kuendelea kutii sheria na alama za barabarani kunakochangiwa na usimamizi mzuri wa askari wa usalama barabarani.
IGP Sirro amesema hayo jana wakati alipofanya kikao kazi na maofisa na askari wa Kikosi cha usalama barabarani wa mikoa ya Kanda maalum ya DSM, Rufiji na mkoa wa Pwani huku akiwataka askari wa Jeshi hilo kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi wanaowahudumia na hasa kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa na kuwasisitiza suala la kutoa huduma bora kwa mteja