INAELEZWA kuwa mabosi wa Simba wamemwaga dola 70,000, ambazo ni sawa na Sh milioni 162 za Kitanzania, kukamilisha usajili wa mshambuliaji wao mpya, Junior Lokosa, mwamba wa Nigeria.

Chanzo makini kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa uzoefu wa mchezaji huyo kwenye michezo ya kimataifa na kupita kwenye timu kubwa za Nigeria na Esperance ya Tunisia, inatajwa kuwapa jeuri viongozi wake ambao hawakutaka auzwe chini ya dola 100,000.

Hata hivyo, baada ya mazungumzo na Simba, menejimenti ya mchezaji huyo ikakubali kulegeza kitita hicho na akamwaga wino Msimbazi kwa dola 70,000 kwa mkataba wa miezi sita, ukiwa na kipengele cha kumuongezea miaka mingine miwili kama ataonyesha uwezo.