Watu wanne wamefariki Dunia Nchini Marekani kufuatia fujo zilizotokea baada ya Wafuasi wa Rais Donald Trump kuvamia Bungeni wakipiga kelele kuwa kura za Trump zimeibiwa na kwamba wanataka Trump abaki madarakani.
Waliofariki ni Mwanamke mmoja ambaye alipigwa risasi pamoja na wenzake watatu, Polisi wamethibitisha na kusema pia wamewakamata zaidi ya Watu 50 kutokana na fujo hizo.
Rais Donald Trump alilazimika kuwatuliza wafuasi wake walioandamana na kuwataka warejee majumbani mwao lakini katika ujumbe wake huo wa video alikazia kuwa uchaguzi ulitawaliwa na wizi>>”najua mnaumia, naumia pia ila tunataka Amani”.