Rais Trump amewasamehe Watu zaidi ya 70 wenye makosa mbalimbali muda mfupi kabla ya kuondoka Ikulu ambapo miongoni mwa waliosamehewa ni Rapper Lil Wayne ambae alikua na hatia ya kumiliki silaha kinyume na sheria ambapo msamaha huu unamfanya anusurike na kifungo cha hadi miaka 10 Jela katika hukumu ambayo ingetolewa January 28 2021.
Lil Wayne amekua upande wa Donald Trump kitambo na hata kwenye kampeni zake amekua akionesha waziwazi kum-support Trump kitendo ambacho kilifanya akosolewe sana na Watu wengi Marekani.
Rapper mwingine aliepata msamaha wa Rais Trump ni Kodak Black ambae wakati msamaha huu wa Rais unatoka bado alikua gerezani ambae pia alikamatwa kwa makosa ya silaha.
Pia, Miongoni mwa wengine waliosamehewa ni pamoja na aliyekuwa mshauri wake mkuu Steve Bannon
Steve Bannon, yeye alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya makosa ya udanganyifu juu ya kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujengea ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico.
Katika kampeni hiyo inadaiwa kuwa Bannon alipokea zaidi ya dola milioni 1, ambazo baadhi ya pesa hizo alizitumia kwa matumizi yake binafsi.