Baraza la Sanaa Taifa ( BASATA ) limemfungia miezi sita msanii wa muziki ‘Gigy Money kutojushughulisha na shughuli zozote za muziki.


Katika taarifa yao, Basata imeeleza kuwa imefikia hatua hiyo baada ya msanii huyo kuvaa nguo zisizo na maadili katika Tamasha la Wasafi ililofanyia Alhamisi iliyopita jijini Dodoma, hivyo kukiuka kanuni za kifungu cha 4(L) cha sheria namba .23 ya mwaka 1984.


Basata imesema adhabu hiyo inaendana na faini ya Sh milioni moja na kwamba adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 64 (1)( a)-(i) za Baraza la Sanaa Tanzania mwaka 2018.