BAADA ya dakika 90 kukamilika sasa ni matuta yataamua nani atakuwa bingwa wa Kombe la Mapinduzi
Simba wanaanza kupiga penalti ya kwanza Uwanja wa Amaan, timu zote zinaomba dua kwa sasa
Shikalo na Beno Kakolanya wanatakiana kila la kheri
Shikalo anakaa langoni na Kahata anakwenda kupiga penalti ya kwanza
Kahata anafunga kwa mguu wa kushoto, Shikalo anafungwa.
Beno anakaa langoni na Tuisila anafunga bao la Kwanza kwa Yanga mguu wa kulia
Shikalo anakaa langoni Kagere anagongesha mwamba.
Beno anakaa langoni Ninja anafunga.
Shikalo anakaa langoni, Mugalu anafunga
Beno anakaa langoni Tonombe anapiga shuti Beno anaokoa
Shikalo anakaa lango Onyango anapiga Shikalo anaokoa
Beno langoni Mauya anafunga
Shikalo langoni Gadiel anafunga
Ntibanzokiza anafunga penalti ya 4 kwa Yanga.
Yanga 4-3 Simba
Bingwa wa Kombe la Mapinduzi ni Yanga