Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameahidi kuwa Serikali ya nchi hiyo itatoa Dola elfu 20 za Kimarekani kusaidia wavuvi katika Mwalo wa Chato mkoani Geita.
Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake hapa nchini Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa China asubuhi hii ametembelea Mwalo wa Chato na kujionea shughuli zinazofanywa na wavuvi hao na kisha kutoa ahadi hiyo.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia samaki wakubwa waliovuliwa katika ziwa Viktoria Waziri Wang Yi ameonesha kufurahishwa na shughuli za uvuvi na kutoa ahadi hiyo.
Awali akitoa taarifa ya shughuli za uvuvi kwenye ziwa Viktoria, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema kuwa, lengo la Serikali ni kuona mazao ya samaki yauzwa moja kwa moja katika soko la China.