Lord Meya Erias Lukwago wa chama cha FD ameweza kutetea kiti chake cha Meya wa jiji la Kampala kwa kuwapiku wapinzani wake 10, akiwemo msanii Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleone na mgombea wa chama cha NUP Nabila Nagayi.

Msimamizi wa kituo cha kupiga kura Ruwaga kitongoji cha jiji la Kampala ndiye aliyekuwa mhusika mkuu katika uhesabu wa kura kwenye matokeo ya uchaguzi wa meya wa jiji la Kampala.


''Ndugu zangu sina cha kuwaambia nina furaha kubwa watu wangu, hapa nyumbani na wakazi wote wa jiji la Kampala asanteni sana, sana''.


Lukwago ameshinda karibu kata zote tano za wilaya ya Kampala kwa mujibu wa matokeo ya mwanzo yaliotolewa katika kata zote.


Wakati huo huo Mahakama kuu mjini Kampala leo inatarajiwa kusikiliza ombi la Robert Kyagulanyi kuachiwa huru na vikosi vya ulinzi vinavyomzuia nyumbani kwake.