Kiungo wa Simba, Clatous Chama ameongeza mkataba wa kuendelea kubaki Msimbazi na kumaliza kabisa tetesi zilizokuwa zikienea kwamba huenda akaondoka kwenye klabu hiyo.

Chama amesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuwatumikia Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara!

Ikiwa mabosi wa Yanga bado wapo kwenye hesabu za kupata saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama inabidi wajipange kuvunja benki kuipata saini ya nyota huyo.

Awali ilikuwa inaelezwa kuwa mwamba huyo mwenye tuzo ya mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/21 yupo kwenye rada za watani hao wa jadi.