MSANII wa Nigeria, Burna Boy, amejumuishwa katika orodha ya nyimbo ambazo zitapigwa wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani,  Joe Biden.

 

Wimbo wa Burna unaojulikana kwa kwa jina ‘Destiny’ utakuwa miongoni mwa nyimbo za wasanii wengine wa kimataifa. Orodha ya nyimbo hizo 46 imeandaliwa katika sherehe ya kuapishwa kwa Biden.

 

“Wasanii na nyimbo zilizochaguliwa zinajumuisha taswira ya kila mtu nchini Marekani. Wanafungua ukurasa mpya na watasaidia kuleta watu pamoja wakati utawala wa Biden na Harris unaanza kazi yake muhimu ya kuunganisha nchi yetu,” taarifa hiyo imesema.

 

Nyimbo nyingine zilizochaguliwa ni pamoja na wasanii wakubwa kama BeyoncĂ© na wimbo wake wa ‘Find Your Way Back’, Kendrick Lamar na Mary J. Blige na wimbo wao wa ‘Now Or Never’, Bob Marley and the Wailers na wimbo wao wa ‘Could You Be Loved’  na wimbo wa ‘Levitating Hit’ wa Dua Lipa.