BEKI chipukizi wa Klabu ya Mtibwa Sugar amesaini rasmi dili la kuitumikia Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Job ambaye amekuwa ni chaguo la kwanza ndani ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Turiani kwa sasa ni mali ya Yanga.

Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Yanga ambayo inaongoza Ligi Kuu Bara.

Anaungana na nyota mwingine mzawa, Bakari Mwamnyeto ambaye ni mzawa pamoja Lamine Moro ambao wote ni mabeki wa kati ndani ya Klabu ya Yanga.

Nyota huyo kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Cong, kesho Uwaja wa Mkapa.