Rais wa Marekani, Donald Trump amekubali kukabidhi madaraka kwa mrithi wake, Joe Bideo baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa Novemba 3, 2020.

 

Trump ametoa taarifa kuhusu makabidhiano ya utawala kwa taratibu zilizowekwa tarehe 20 Januari lakini ameendelea kusisitiza madai yake ya kuibiwa kura.

 

“Licha ya kwamba sikubaliani na matokeo ya uchaguzi, na ukweli utabaki kuwa uleule, ingawa makabidhiano ya madaraka yataenda kwa amani kama yalivyopangwa kufanyika Januari 20,” alisema, katika taarifa iliyochapishwa na msemaji wake katika akaunti ya Twitter.

 

“Nimesema siku zote tutaedelea na mapambano yetu kuhakikisha kuwa kura zote zilipigwa kihalali.”

 

Wakati hili likiwakilisha awamu ya kwanza ya urais wenye historia ya mafanikio, huu ni mwanzo tu wa mapambano ya kuifanya Marekani kuwa nzuri tena, aliongeza. Zaidi ya kesi 60 za kikosi cha kampeni cha Trump zilishindwa mwezi Novemba.