ALIYEKUWA mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo na mshauri wa chama hicho, Bernard Membe, ametangaza rasmi jana Desemba Mosi kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama hicho.


Akiwa nyumbani kwake kijijini Rondo Chiponda, Wilaya ya Mtama Mkoa wa Lindi, ameeleza kuwa hajafanya uamuzi huo kwa shinikizo lolote na kwamba kwa sasa atakuwa mshauri wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi ya Tanzania na kupigania demokrasia ya kweli.