Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limemfungia miezi 6, Msanii Gigy Money kujihusisha na sanaa ndani na nje ya Tanzania na kulipa faini ya Tsh milioni 1, mara baada ya kupanda jukwaani mnamo Januari 1, 2021 jijini Dodoma akiwa amevaa dela kisha kulivua na kuonyesha mwili wake.