AJALI  imetokea majira ya saa 11 alfajiri ya leo Jumamosi, Januari 16, 2021, baada ya basi la abiria, mali ya Kampuni ya Saratoga, lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na gari dogo la abiria (Hiace) maeneo ya Mbezi jijini Dar.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, hakuna kifo kilichotokea ispokuwa kuna majeruhi ambao ni pamoja na kondakta wa basi hilo ambaye amevunjika mguu.


 
Aidha, Hiace hiyo imeharibika nyang’anyang’a huku dereva wake akisalimika na kukimbia eneo la tukio kwenda kusikojulikana. Kwa taarifa zaidi endelea kufuatia taarifa zetu