Treni ya abiria iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Bara (Mwanza, Mpanda na Kigoma kupitia Tabora) imepata ajali Wilayani Bahi umbali wa kilometa 40 kutoka Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amethibitisha.

“Treni ilikuwa na Watu zaidi ya 700, kuna mvua zinanyesha sana, bado hatujajua chanzo cha ajali ila kichwa kimeanguka, taarifa za awali zinaonesha Mfanyakazi wetu mmoja amefariki na abiria wawili wamefariki, nilikuwa likizo nimeikatisha naelekea eneo la tukio”- Kadogosa

“Tunaandaa Mabasi ya kwenda kuchukua abiria pale wawapeleke Manyoni, kuna Treni yetu ya abiria inatoka Bara, wanaoendelea na usafiri Bara waingie huko waendelee na safari, na waliokuwa wanatoka Bara kuelekea Dar Es Salaam waingie kwenye Mabasi wawalete DSM”-Kadogosa.