KIUNGO mkabaji wa klabu ya Simba, Jonas Mkude leo Januari 21, 2021 amejitokeza rasmi na kuomba radhi kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zilizokuwa zikimkabili.

 

Mkude ambaye ni mchezaji Mwandamizi wa kikosi cha Simba hajaichezea Simba tangu  Desemba 23, mwaka jana alipocheza mchezo wa michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

 

Akiomba radhi hiyo Mkude amesema: “Tumeumbwa kukosea lakini haimaanishi nitakosea tena, mimi ni Mwanasimba mwenzenu na klabu hii ni sehemu ya maisha yangu.

“Naamini wachezaji wenzangu, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na mashabiki mtanielewa na kunisamehe,”