ALIYEKUWA mpinzani mkuu kwenye uchaguzi wa urais nchini Uganda Bobi Wine amesema atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi uliomrejesha madarakani rais Yoweri Museveni huku akiwataka wafuasi wake kujizuia na machafuko.
Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi amesema leo hatua hiyo inachukuliwa baada ya kujadiliana na uongozi wa juu wa chama chake cha National Unity Platform NUP.
Wine pamoja na chama chake wanadai kumefanyika udanganyifu wakati wa uchaguzi huo wa Januari 14,
Kiongozi huyo wa muda mrefu mwenye miaka 76 amechaguliwa tena kwa asilimia 58.6 ya kura zote na kufuatiwa na Wine aliyepata asilimia 34.6.