Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupungua kwa bei ya Petroli kwa Sh. 31 kwa lita moja mwezi huu.

Wakati Petrol ikipungua, bei ya Dizeli imeongezeka kwa Sh. 9 wakati ile ya mafuta ya taa ikipanda kwa Sh. 29 kwa lita moja.

Mabadiliko ya bei hizo za jumla na rejareja ni kwa mafuta yaliyopokelewa Bandari ya DSM, mabadiliko hayo yametajwa kusababishwa na kinachoendelea katika soko la dunia na gharama za usafirishaji.

Bei ya jumla ya Petroli imepungua kwa Sh. 31.1 kwa lita sawa wakati Dizeli ikiongezeka kwa Sh.8.74 na mafuta ya taa yakiongezeka kwa Sh.29.31 kwa lita moja.

Kwa mujibu wa EWURA bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia leo January 7, 2020, kutokana na hali hiyo, EWURA imesema kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta kwa kuzingatia bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na kanuni ilyopitishwa

“Pia vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei katika mabango yanayoonekana bayana yakiwa na punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika,” ilieleza taarifa hiyo. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani, EWURA imesema ni kosa kuuza mafuta bila kuweka bango la bei linaloonekana vizuri kwa wateja” EWURA

“Adhabu kali itatolewa kwa kituo ambacho hakitotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika ikiwamo kutoa risiti za mauzo za kielektroniki na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita,” EWURA