BARAZA la Sanaa Taifa ( BASATA ) limewataka wasanii wote ambao watatumbuiza katika Tamasha la ‘Tumewasha’ linaloendeshwa na Wasafi Media kuhakikisha wamesajiliwa na baraza hilo ili kuwa na uhalali wa kupanda jukwaani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari hii jana, Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Wasafi Media’,  Naseeb Nyange ‘Diamond Platnumz’,  amesema wako tayari kufuata agizo hilo ili kuepuka kufungiwa kwa tamasha hilo litakalohusisha wasanii wa ndani na nje ya nchi.

 

 

“Tunatamani kuwa na wasanii wote, hivyo kwa wasanii ambao hawajasajiliwa na Basata wasajiliwe ili tuwe nao,” amesema Diamond Platnumz.

 

 

Kuelekea tamasha hilo litakalofanyika Januari 30, 2020, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam,  Diamond amesema wasanii ambao hawajasajiliwa na wako tayari kufanya hivyo atawasaidia kujisajili kupitia tamasha hilo kwa angalizo  la ‘Tumewasha Tour’