Uongozi wa Simba umesema kuwa nyota wao mpya Bernard Morrison hasumbuliwi na tatizo lolote bado yupo imara licha ya habari kueleza kuwa anaumwa.


Leo Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mchezaji huyo ni mzima na hana tatizo.


“Morrison ni mchezaji hana tatizo yupo fiti na ataonekana uwanjani hivi karibuni hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu mchezaji wetu,” Barbara Gonzalez