Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani limewasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Donald Trump na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la pili la kihistoria.

Wawakilishi tisa walioteuliwa kuongoza mchakato huo wamewasilisha shtaka moja pekee linalomtuhumu Trump ambalo ni la ‘kuchochea uasi’ baada ya wafuasi wake kuvamia majengo ya bunge mjini Washington mapema mwezi huu.

Kuwasilishwa kwa hati hiyo ya mashtaka iliyoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na Chama cha Democrat Januari 13, kunafungua njia ya kuanza kwa shauri dhidi ya Trump katika wiki ya pili ya mwezi Februari.