DHORUBA ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi kumbania matunzo baba yake mzazi mzee Abdul Juma, haijatulia, Risasi limebaini.


Mbali na baadhi ya watu kuendelea kumtuhumu Mondi kuwa hamjali baba yake, mzigo wa lawama ungali begani kwa mama yake Sanura Kassim ‘mama Dangote.’


Kisa kibichi kilichochokonoa mazito hivi karibuni ni picha za baba Mondi kuchapishwa kwenye gazeti dada la hili Ijumaa Wikienda likimuonesha mzazi huyo wa Mondi akiwa amebeba mfuko wa kiroba huku akidandia daladala.


Maelezo yaliyopatikana nyuma ya picha hiyo ni kwamba mzazi huyo wa msanii Mondi amekuwa akiishi maisha ya uchuuzi wa viatu ambapo wengi walisema kutokana na hali nono ya mwanaye hawakutarajia baba yake aishi maisha kama hayo ya kubangaiza.