BLevo Fundi Manyumba @officialbabalevo ametangaza Vita na mtu yoyote atakae thubutu kumsema vibaya au kumtukana @diamondplatnumz, na kudai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuchezea mkate wake wa kila siku .


@officialbabalevo amedai kuwa Diamond amegharamia zaidi ya Milion 28 kwa ajili ya Video yake ya #Shusha, bila kudai kurudishiwa hata Senti Tano . Hivyo kitendo hicho kinaonyesha mapenzi makubwa aliyonayo juu yake na namna alivyoamua kumsaidia kwenye muziki na maisha yake kwa ujumla .


"Natangaza rasmi, ukimsema @diamondplatnumz vibaya ujue umeingia kwenye Vita rasmi na mimi. Sijali waniite chawa, Mende, kunguni au papasi, Cha msingi ni Boss wangu na ananilipa mshahara wa mamilioni " - @officialbabalevo