Amos Rudovick (39) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Dastan Amos (13) kwa kumchapa na fimbo ambazo zilipelekea kifo chake


Uchunguzi wa Madaktari umeonesha kipigo hicho kilimvunja shingo na Uti wa Mgongo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Revocatus Malimi, amesema tukio lilitokea Januari 02, 2021 Ibale Wilayani Kyerwa


Dastan ambaye ni Mwanafunzi wa Darasa la Nne alipigwa na Baba yake kwa sababu alienda kutembea bila idhini ya Wazazi wake, na kurejea nyumbani saa tisa alasiri