Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Aggrey Morris ameagwa kishujaa hii leo uwanja wa Mkapa akitundika daluga rasmi kunako Taifa Stars wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya DR Congo. Morris amepewa jezi, mpira na hundi yenye thamani ya shilingi milioni tano.