Rapper @younglunya ambae ni miongoni mwa rapper's wa kizazi kipya wanaofanya vizuri kwenye ramani ya muziki wa rap hapa nchini, amefunguka kuwahi kuwa miongoni mwa wasanii waliokuwepo kwenye kituo cha kulea vipaji, Mkubwa na Wanawe.

Akizungumza kwenye kipindi cha Empire cha E FM Radio, #Lunya amesema kuwa alikwenda hapo na rafiki yake ambae anaamini alikuwa mkali kuliko yeye lakini @mkubwafellatmk alimchagua yeye.

Sababu ya kuchaguliwa, @younglunya ameeleza kuwa #Fella alisema anaona kitu kwake.

Katika hatua nyingi, #Lunya alifunguka kuhusu ukaribu wake na #Mabantu ambapo ameeleza, wakati anaanza kwenda kwaajili ya Mazoezi (Mkubwa na Wanawe) na hapo ndipo alikutana na #Mabantu wakiwa wadogo sana. Pia ameeleza kuwashirikisha #Mabantu katika ngoma zake zijazo baada ya wao kumshirikisha katika nyimbo zao mbili.

“Kuna kazi nimefanya nao lakini mimi nilikuwa nimeshaweka mipango yangu ya mwaka mzima” alisema @younglunya ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake uitwao "Fimbo"