SIYO Namungo FC tena, safari hii jina la beki wa kati na nahodha wa zamani wa Yanga Kelvin Yondani limeibuka kwenye usajili wa Coastal Union ya mkoani Tanga.

 

Yondani kwenye usajili mkubwa wa msimu huu, alitajwa kuwepo kwenye mipango ya kuwaniwa na Namungo FC kabla ya dili hilo kupotea na kubaki bila ya kuwepo kwenye timu yoyote inayoshiriki ligi.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, beki huyo anatajwa kuwaniwa na Coastal inayofundishwa na Juma Mgunda ili kwenda kuimarisha eneo la ulinzi baada ya kuondokewa na walinzi Bakari Mwamnyeto aliyetimkia Yanga na Ibrahim Ame aliyetua Simba.

Stori na Wilbert Molandi, Dares Salaam