Ligi kuu ya Soka ya Vodacom Tanzania bara kuendelea leo Disemba 6 kwa mechi 3 kuchezwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini.


Vinara wa ligi hiyo Yanga SC watakuwa uwanja wa Mkapa kuwakaribisha Ruvu Shooting, mechi itakayochezwa kuanzia saa 1:00 usiku. Yanga wanataka alama 3 ili kuzidi kujikita kileleni wakati Ruvu nao wanataka alama 3 ili wazidi kusogea nafasi za juu.


Mchezo mwingine ni ule utakaowakutanisha Mtibwa Sugar Vs Mwadui huku Ihefu ikiwakaribisha JKT Tanzania ambapo hii ni vita ya kutoka nafasi za chini katika msimamo kwani timu zote zipo nafasi za chini na zikiwa zinapambana kusogea juu kuepuka kushuka daraja.