MWAKA 2020, unakwenda kumalizika kwa uzuri zaidi kwa staa wa muziki wa Nigeria, Wizkid mara baada ya juzi Alhamisi kutajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Music Of Black Origin (MOBO) kutoka England.

 

Wizkid anatwaa tuzo hiyo ikiwa ni mwezi mmoja tangu aingize albamu yake ya Made In Lagos, ambayo hadi hivi sasa inatajwa kuwa moja kati ya albamu bora barani Afrika ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka huu.



Wizkid alitajwa kama mshindi wa kipengele cha Msanii Bora wa Afrika (Best African Act), huku wakali wengine kama Burna Boy akishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kimataifa (Best International Act) akiwaangusha Drake, Megan Thee Stallion, Pope Smoke, Lil Baby, Rema na wengin.
 
OPEN IN BROWSER