Mkurugenzi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), David Palangyo amekuwa wa kwanza kuonja joto ya jiwe baada ya kusimamishwa kazi na Waziri wa Maji Jumaa Aweso.

Aweso amemsimamisha kazi Mkurugenzi huyo na kumuagiza Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga kumbadilisha kituo cha kazi Palangyo.

Aweso ambaye ameapishwa jana na Rais John Magufuli amesema haridhishwi na utendaji kazi Palangyo kwa kile alichodai kuwa Jiji la Dodoma linahitaji mtendaji mwenye kasi zaidi na kwamba Palangyo asubiri kupangiwa kazi nyingine.