Jeshi la Polisi Wilayani Musoma Mkoani Mara linawashikilia watu wanne kwa kujihusisha na Mtandao wa Kampuni ya QNET na kutapeli watu.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naano amesema, uchunguzi umebaini watu wengi wametapeliwa huku akimtaja mstaafu mmoja wa manispaa na familia yake ambaye ametapeliwa Tsh. milioni 15.

Aidha, imebainika kuwa, watu wengi waliotapeliwa wameshindwa kufika kwa Vyombo vya Dola kutoa taarifa na pia mtandao huo hauna muwakilishi hapa nchini.

Uchunguzi unaendelea kwa ofisi nne za QNET ambazo zipo Mjini Musoma.