WASTARA kwa uchungu aandika maneno mazito kwa marehemu SAJUKI na kuwaliza watu wengi, Akiri kuteseka

"Zimebakia siku 6 tu utimize miaka 8 tokea ufariki na kuniacha peke yangu kwenye midomo ya mamba tasa

Nina maswali mengi sana nataka nikuulize lakini atanijibu nani ila uliwezaje kunielewa kirahisi kuliko mtu yoyote hapa duniani hata familia yangu ainielewi bado mpka leo ila wewe uliweza nauliza uliwezaje 😢😢😢

Kwenye dunia kuna watu wapo tu kuumiza watu wenye mapungufu tayari wanawaongezea upungufu mwingine na kuwatia unyonge na udhaifu wakija wanatumia vigezo vya mapungufu yaliyopo mjane yatima mlemavu nataka kumlea nataka kumfariji maneno mengiìi uliyeweza ni wewe peke yako japo ulisema siku ukifika yupo mwingine atakuja kuziba nafas yako ila ulinidanganya hakuna mpaka sasa nimetafuta sana sijamuona hata robo yake tu unaefanana nae hayupo wananichapa tu kwa fimbo ya mapungufu yangu na ukiwa wangu i ujane wangu uyatima wangu ulemavu wangu

Hìi inanitesa sana i wish uje hata mara moja nikushtakie wanachonifanyia

Tal 2/1/2021 unafkisha miaka 8 inshaAllah mungu anipe fursa na aniwezeshe nikuombee dua kubwa wewe na wazazi wangu wawili kama nilivyofanya miaka yote iliyopita

MUNGU akusamehe kila ulipoteleza akujaalie nuru kaburini mwako aondoshe mchanga mzito kaburini kwako..AMIIN AMIIN AMIIN AMIIN" Wastara


Tazama Hapa Chini: