Jopo la wajumbe maalumu lenye nguvu ya kumchagua rais wa Marekani, limemuidhinisha rasmi Joe Biden kuwa rais ajae wa urais wa taifa hilo, na hivyo kufunga milango kwa mpinzani wake, katika jitihada zake za kisheria za kuyageuza matokeo ya uchaguzi wa 2020.

Wakati Biden akipiga kampeni ya kuunganisha taifa, baada ya uchaguzi uliowagawa Wamarekani, wajumbe kutoka majimbo yote jana Jumatatu, wamekutana kutoa hakikisho la ushindi wake, kwa jimbo la Califonia kumsogeza Biden kwa matokeo ya kupindukia kura za majimbo 270. 

Hatua hiyo maana yake ni kumsafishia njia sasa kuekea kuingia katika ofisi za Ikulu ya Marekani Januari 20. 

Uchaguzi wa Marekani wa Novemba 3, uliingia katika kizungumkuti tangu kumalizia kwake, baada ya Rais Donald Trump pasipo kuwa na ushahidi kuendelea kutangaza na kulalamika kwamba kulifanyika udanganyifu mkubwa.