Samirah Yusuph
Busega. Wahamiaji haramu 34 raia wa Ethiopia wamekamatwa katika kitongoji cha Mwalukonge kijiji cha Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu.

Wahamiaji hao wameingia nchini kupitia mpaka wa Sirari Mkoani Mara ambapo afisa uhamiaji mkoa wa simiyu  Mariam Mwanzalima aliviambia vyombo vya habari kuwa wamewakamata watu hao mashambani.

"Kwa mujibu wa maelezo yao walikuwa wanaelekea Malawi  na walikuwa  wenyeji watatu ambao ni wakenya wawili na mtanzania mmoja ambao walikuwa wanawasafirisha kwa kutumia mchomoko (noah).

Wakaingia mtafaruku na wenyeji wao baada ya kuwashusha kwenye gari na kutaka kuwapandisha mtumbwi ndipo walipoanza ugomvi na kundi hili lilikimbia kuelekea mashambani.

Huko tulipata taarifa na askari wetu kwa kishirikiana na askari wa jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuwakamata,"

Mwisho.