Watu kadhaa wamejeruhiwa wakati ambapo vikosi vya usalama vilikuwa vinawatawanya wafuasi wa mgombea urais wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, eneo la Kayunga, karibu na Kampala.

Watu wanne wamejeruhiwa katika kampeni yake mmoja wao akitambuliwa kama mtayarishaji muziki Dan Magic ambaye amepata jeraha la usoni


Afisa wa polisi ambaye pia ni sehemu ya maafisa wa usalama wanaomlinda mgombea huyo wa urais kufuatia agizo la Tume ya Uchaguzi pia naye amepata majeraha ya kichwa.


Takriban wiki mbili zilizopita, watu 54 waliaga dunia katika maandamano ya kudai Bobi Wine aachiwe huru baada ya kukamatwa katika mkutano wa kampeni.


Bobi Wine baadaye alishitakiwa kwa kukiuka hatua za kukabiliana na virusi vya corona na kuachiwa huru kwa dhamana.