WATUMIAJI wa  mawasiliano ya Whatsapp katika simu za  iPhone 4 au simu za zamani za Android hawataweza kutumia vyema huduma hiyo ifikapo Januaryi 1, 2021.

 

Mtandao huo unaomilikiwa na  Facebook hautafanya kazi katika simu hizo za toleo la 9 (iOS 9) la Apple tangu 2015.

 

Watu wasiotumia matoleo ya Apple kwa matoleo ya zamani nao wataathirika iwapo bado wanatumia Android 4.0.3.  Kwa kifupi watumiaji wa zana hizi watapoteza mawasiliano na habari zao.

 

Toleo la iOS 9 lilikuwa la mwisho ambalo simu za  iPhone 4 ziliweza kupokea mawasiliano, na matoleo yaliyofuata yakiweza kuimarisha utendaji kazi wa matoleo yaliyofuata.  Apple ilitoa toleo la  iOS 14 mnamo  Septemba 2020.Matoleo kama  4s, 5s, 5s, 5C, 6 na 6s yanaweza kuendelezwa ili kupata mawasiliano ya WhatsApp katika simu.

 

Hatua hiyo ya kuacha kuhudumia zana za zamani ni mbinu ya kila mara ya wamiliki wa app ni kupata nguvu zaidi ya kuendeleza bidhaa hiyo kwa ajili ya watumiaji wengi zaidi ambao hawana simu za kisasa.

 

WhatsApp ni moja ya  apps maarufu zaidi duniani, ikiwa na watumiaji bilioni 1.5.  Pia WhatsApp bado ni maarufu duniani ambako simu za bei ndogo na za kisasa bado zinatumika.

 

Watumiaji wanaohofia kupoteza mawasiliano na WhatsApp  wachunguze iwapo mipangilio ya simu zao iko sambamba na  iOS 9 au Android 4.0.3.

 

Kwa simu ambazo haziwezi kupangwa sambamba na zana za kisasa, app itaacha kufanya kazi asubuhi ya kwanza ya mwaka 2021.