Mtumishi wa Mungu Nabii Tito amesema kwa sasa yupo katika kampeni nzito inayoitwa hatua ya kwenda mbinguni na kampeni hiyo ipo kwa ajili ya kupinga vita mitume na manabii matapeli.Nabii Tito amesema atawataja mitume na manabii hao kwa Serikali ili iwashughulikie kwani wanatumia dini kuwapigia watu na sio kuhubiri kuhusu kuacha dhambi.


"Baada ya kumaliza kampeni ya chama na kufanya nchi iwe ya kijani, sasa hivi nipo katika kampeni kali sana inayoitwa hatua ya kwenda mbinguni, hiyo ni kampeni ya kupinga vita mitume na manabii matapeli" 


"Sitaki kabisa kuzungumzia mambo mengine zaidi ya kupiga vita matapeli,  wanatumia dini kuwapiga watu na kuuza vitu, nataka niwataje wote ili Serikali ya kijani iwashughulikie maana hawahubiri watu waache dhambi bali wanahubiri ili wapate vitu" ameeleza Nabii Tito 


Aidha amesema yupo katika harakati za watu waache dhambi ili magonjwa yote yakimbie, pia amewataka vijana waokoke kwani ukimwi kwa Kristo hauna nguvu na takwimu zimeongezeka kwa sababu watenda dhambi wameongezeka.