SINTOFAHAMU ya ugomvi wa ndugu wawili, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ na Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, inaendelea. Kwa mujibu wa watu wa karibu wa wawili hao, chuki iliyojengeka kati yao, sasa imefika pabaya.

Imedaiwa kwamba, kila kukicha hali ya uhusiano wao kama ndugu ambao ni dada hao wa staa wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, inazidi kuwa mbaya na inaonesha waziwazi kwamba hawapo sawa kama zamani.

Chanzo chetu kinafunua kwamba, ni kweli ndugu hao hawako sawa kama walivyokuwa huko nyuma na ndicho hasa kilichosababisha Esma kushindwa kwenda kwenye arobaini ya mtoto wa Darleen iliyofanyika hivi karibuni nyumbani kwake, Mbezi-Beach jijini Dar.

“Asikudanganye mtu, chuki ya hawa watu inaongezeka kama joto la Dar. Unaambiwa bado wapo kwenye bifu hatari sana. “Unaambiwa hata huyo kaka yao Nasibu (Diamond) amejaribu sana kuwaweka pamoja, lakini imeshindikana kabisa.

“Kila kukicha ni chuki tu inaendelea kuongezeka kati yao,” kilisema chanzo hicho kilicho ndani ya familia hiyo. Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limefanya jitihada za kutaka kuwakutanisha Esma na Darleen, lakini kila mmoja hakutaka kusikia jambo hilo.

Katika mazungumzo na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Darleen amesisitiza kwamba, kwa upande wake yeye hana tatizo lolote na Esma.

Darleen anasema kuwa, kitendo cha Esma kutoonekana kwenye arobaini ya mtoto wake, wala isiwe sababu. “Mimi ningeomba sana watu wasikariri vitu.

Mimi sina tatizo kabisa na Esma. Watu watambue sisi ni ndugu kabisa na wala siyo marafi ki kama wanavyotuchukulia. “Kama Esma hakuja kwenye shughuli yangu, basi watu wajue wazi alitingwa,” anasema Darleen ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na ‘first lady’ wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Kwa upande wake, Esma, katika mazungumzo na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuhusu ugomvi wake na Darleen, aliomba atafutwe wakati mwingine kwani kwa sasa yupo bize kidogo na majukumu binafsi.

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, kama chombo cha habari, tunawataka ndugu hao kumaliza tofauti zao kama inavyoelezwa na baadhi ya ndugu zao, jamaa na marafiki.

Esma na Darleen, kila mmoja ana baba yake. Darleen baba yake ni Mzee Abdul Jumaa (Baba D), wakati Esma baba yake ni Mzee Khan. Darleen na Esma ni ndugu kwani wote ni damu moja na Diamond ambapo Esma ni kwa upande wa mama na Darleen ni kwa upande wa baba.


STORI: IMELDA MTEMA, DAR