Aliyekuwa mume wa msanii Shilole, Uchebe amesema sio kila anachofanya mtandaoni ni kwa ajili ya kumuumiza msanii huyo bali ni kwa ajili ya maisha yake.

Kauli ya Uchebe inakuja baada ya hivi karibuni kusambaa kwa video yake anayoonekana akicheza kitandani na mrembo mmoja ambaye hakutambulika kwa haraka kitu ambacho hakikuzoeleka kutoka kwake.


“Siwezi kuposti kitu kwa ajili ya kumshambulia mtu, nafanya kile ambacho naweza kufanya katika maisha yangu,” amesema Uchebe akiwaambia Waandishi kwenye usiku wa Tuzo za Tanzania Consumers Choice Awards zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Desemba 14.


Ikumbukwe Uchebe alimuoa Shilole mwaka 2017, wakaachana mapema mwaka huu kwa kile #Shilole alichodai kuwa, alikuwa akipigwa na kuteswa sana katika ndoa yake.